New inheritance law

Together with the KIKUHAMI Taskforce led by WiLDAF, WLAC has participated in drafting a bill for a new inheritance law. This law would ensure inheritance rights for all, eliminating the customary laws that deny women such rights. Additionally, it would consider guaranteeing a share of the matrimonial assets before they are subjected to division. These are essential steps recommended by #CEDAW committee that we hope the government will acknowledge so that Tanzania’s many female widows can finally attain justice.
___

WLAC kwa kushirikiana na Kikosi cha Kutetea Haki za Mirathi (KIKUHAMI) imeshiriki katika kuandaa muswada wa Sheria ya Mirathi. Mswada huu umezingatia haki ya kurithi kwa watu wote na kuondoa Sheria ya Mirathi ya Kimila ambayo inawanyima wanawake haki ya urithi. Vilevile,mswada huu umezingatia mchango wa mwenza katika mali ya ndoa kabla mali hiyo haijagawanywa kama sehemu ya mali za marehemu. Hii hatua muhimu katika kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Mkataba wa CEDAW na ni matumaini yetu kwamba serikali itaukubali na kuupitisha mswada huo.