+255 22 266 4051 wlac@wlac.or.tz
MIPANGO Upatikanaji wa Haki

Kuimarisha Upatikanaji wa Haki na Utetezi wa Maboresho ya Sera

Upatikanaji wa haki bado ni changamoto kubwa kwa wanawake na wasichana, hususan manusura wa ukatili, ubaguzi, na kutengwa kijamii na kiuchumi. Vikwazo kama vile upatikanaji mdogo wa huduma bora za msaada wa kisheria, uelewa mdogo wa haki za kisheria, mifumo ya haki isiyozingatia usawa wa kijinsia, pamoja na mila na desturi kandamizi vinaendelea kudhoofisha uwezo wa wanawake kutafuta na kupata haki nchini Tanzania.

Katika eneo hili la kimkakati, WLAC inalenga kuimarisha upatikanaji wa haki na kutetea maboresho ya sera yanayozingatia usawa wa kijinsia ili kuendeleza haki za wanawake na usawa wa kijinsia. WLAC itaboresha upatikanaji wa huduma bora za msaada wa kisheria zinazomweka manusura mbele, kuimarisha mifumo ya ulinzi na fidia kwa manusura wa ukiukwaji wa haki, na kuwawezesha wanawake na wasichana kwa kuwapatia maarifa na ujasiri wa kudai haki zao za kisheria kupitia mipango ya uhamasishaji wa kisheria ngazi ya jamii.