+255 22 266 4051 wlac@wlac.or.tz
MIPANGO Uhamasishaji wa Jamii

KUHUSU HAKI ZA KIRAIA NA KIJAMII-KIUCHUMI


Kuimarisha uelewa na ushiriki wa jamii kuhusu usawa wa kijinsia na haki za kijamii-kiuchumi

Uelewa mdogo kuhusu haki za kisheria, kiraia, na kijamii-kiuchumi unaendelea kuwazuia wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika jamii na kudai stahiki zao. Mila na desturi kandamizi, mitazamo ya kijinsia iliyojengeka kimakosa, pamoja na upotoshaji wa taarifa vinaendelea kupunguza ushiriki wa jamii katika kuendeleza usawa wa kijinsia na uwajibikaji.

WLAC inalenga kuimarisha uelewa na ushiriki wa jamii kuhusu usawa wa kijinsia na haki za kijamii-kiuchumi. Kupitia kampeni maalum za uhamasishaji, elimu ya uraia, na mipango shirikishi, WLAC itawawezesha wanawake, wanaume, vijana, na viongozi wa jamii kuelewa na kutumia haki zao. Hatua hizi pia zitakuza majadiliano jumuishi, kupinga mila na desturi za kibaguzi, na kuhamasisha ushiriki hai katika utawala na michakato ya maamuzi ya kijamii na kiuchumi.

Kupitia kuongeza uelewa wa haki na kuimarisha ushiriki wa jamii, WLAC inalenga kujenga jamii zilizo na uelewa, uwezo, na uthubutu wa kuchukua hatua zinazounga mkono usawa wa kijinsia, kulinda haki za wanawake na wasichana, na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi yaliyo sawa.

Kuimarisha sauti za wanawake kuhusu haki za ardhi


Kuwawezesha wanawake huanza na uelewa:
Vifaa vya IEC kuhusu haki za ardhi, tunapanda mbegu za maarifa zinazowasaidia wanawake kudai, kulinda, na kumiliki kile ambacho ni haki yao.